Matamshi ya Kristo wa Siku za Mwisho | “Jinsi ya Kuhudumu kwa Upatanifu na Mapenzi ya Mungu”

2019-02-21 1

Matamshi ya Kristo wa Siku za Mwisho | “Jinsi ya Kuhudumu kwa Upatanifu na Mapenzi ya Mungu”

Mwenyezi Mungu anasema, “Ikiwa ungependa kutumikia mapenzi ya Mungu, ni lazima kwanza ufahamu ni watu wa aina gani wanapendwa na Mungu, ni watu wa aina gani wanachukiwa na Mungu, ni watu wa aina gani wanafanywa kuwa kamili na Mungu, na ni watu wa aina gani wana sifa zinazostahili kumhudumia Mungu. Hiki ni kiasi kidogo zaidi unachopaswa kujiandaa nacho. Isitoshe, unapaswa kujua malengo ya kazi ya Mungu, na kazi ambayo Mungu Ataitenda hapa na wakati huu. Baada ya kufahamu haya, na kupitia kwa mwongozo wa maneno ya Mungu, kwanza utaingia, na kupokea agizo la Mungu kwanza. Unapopata uzoefu wa kweli kwa msingi wa maneno ya Mungu, na unapojua kweli kazi ya Mungu, utakuwa umehitimu kumhudumia Mungu. Na unapomhudumia ndipo Mungu atayapa nuru macho yako ya kiroho, na kukuruhusu kuwa na ufahamu mkubwa zaidi wa kazi Yake na kuiona dhahiri zaidi. Ukiingia katika ukweli huu, uzoefu wako utakuwa wa kina zaidi na wa kweli, na wale wote ambao wamepata uzoefu wa aina hiyo wataweza kutembea miongoni mwa makanisa mengi na kuwatolea ndugu zao, kila upande ukipokea kutoka kwa uwezo wa wengine ili upungufu wao wenyewe, na kupata maarifa mengi zaidi ndani ya roho zao. Ni baada tu ya kutimiza matokeo haya ndipo utakapoweza kutumikia mapenzi ya Mungu na kufanywa mkamilifu na Mungu wakati wa kufanya huduma yako.”

Tazama zaidi:
Matamshi ya Kristo wa Siku za Mwisho | “Kumjua Mungu Ndiyo Njia ya Kumcha Mungu na Kuepuka Maovu” https://sw.kingdomsalvation.org/videos/fearing-God-and-shunning-evil-word.html
Matamshi ya Mungu “Namna ya Kujua Tabia ya Mungu na Matokeo ya Kazi Yake” Sehemu ya Pili https://sw.godfootsteps.org/videos/know-God-s-disposition-2-word.html

Umeme wa Mashariki, Kanisa la Mwenyezi Mungu lilianzishwa kwa sababu ya kuonekana na kazi ya Mwenyezi Mungu, ujio wa pili wa Bwana Yesu, Kristo wa siku za mwisho. Linashirikisha wale wote ambao wanaikubali kazi ya Mwenyezi Mungu katika siku za mwisho na ambao wameshindwa na kuokolewa kwa maneno Yake. Liliasisiwa kikamilifu na Mwenyezi Mungu mwenyewe na linaongozwa naye kama Mchungaji. Kwa hakika halikuanzishwa na mtu. Kristo ni ukweli, njia, na uzima. Kondoo wa Mungu husikia sauti ya Mungu. Mradi unasoma maneno ya Mwenyezi Mungu, utaona kuwa Mungu ameonekana.

Kauli Maalum: Uzalishaji huu wa video ulitengenezwa kama mradi usio wa faida na Kanisa la Mwenyezi Mungu. Video hii isisambazwe kwa mtu mwingine kwa minajili ya faida, na ni matumaini yetu kwamba kila mtu atashiriki kuigawa na kuisambaza hadharani. Wakati unapoisambaza, tafadhali sisitiza chanzo chake. Bila ridhaa ya Kanisa la Mwenyezi Mungu, hakuna shirika, kundi la kijamii, au mtu binafsi anayeweza kubadilisha au kuhudhurisha visivyo maudhui ya video hii.

Injili ya Kushuka kwa Ufalme: https://sw.kingdomsalvation.org/
Kanisa la Mwenyezi Mungu: https://sw.godfootsteps.org/